Breaking

Thursday 5 May 2022

SERIKALI YATANGAZA RASMI NAFASI ZA AJIRA YA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022, TAZAMA JINSI YA KUTUMA MAOMBI HAPA



Serikali imetangaza ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) George Simbachawene amesema Watanzania wote wenye sifa wanaruhusiwa kutuma maombi na wafuate vigezo vilivyo ainishwa.

Aidha, amesema katika mchakato huo wa kutuma maombi, hakuna kiasi chochote cha fedha kinacho tozwa na wananchi wawe makini ili kuepuka kutapeliwa.

Maombi haya yanapatikana katika tovuti zifuatazo:-

1. www.tamisemi.go.tz

2. www.nbs.go.tz

3.
www.ocgs.go.tz


Tumia hii link katika kutuma maombi ya Ajira ya Sensa https://ajira.nbs.go.tz

Maombi yatumwe kuanzia tarehe 5-19 Mei, 2022 kama ilivyo elekezwa kwenye fomu za maombi.

Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa


















Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages