Breaking

Friday 27 May 2022

BRELA KUFUTA MAKAMPUNI 5,676 YALIYOSHINDWA KUKIDHI VIGEZO, TAZAMA ORODHA HAPA



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imekusudia kufuta Makampuni 5,676 ambayo yameshindwa kukidhi vigezo vya kisheria ikiwemo kutokuwasilisha Taarifa za Mwaka za Kampuni.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 27 Mei, 2022 katika ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi za taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

Nyaisa amesema baadhi ya watu wamekuwa wakisajili na kushikilia majina na baadaye kuuziana.

"Tumegundua kuna hiyo tabia, watu wanauziana majina, mtu anashikilia mtu akilihitaji wanakubaluana ndiyo maana tumekuja na hili suala la kufuta ili watu waweze kuomba hayo majina," amesema.


Amezitaja sababu nyingine zinazofanya kampuni kuonekana hazifanyi biashara ni pamoja na, kukosa mtaji wa biashara, kuelemewa na migogoro baina ya wamiliki, kushindwa kutimiza malengo yaliyokusudiwa na hivyo kutokuwa na sababu ya kuendelea na uendeshaji wakampuni na kutokuwa na uelewa kuhusu wajibu wa Wakurugenzi na Wamiliki wa Kampuni.

FUNGUA LINK HIIORODHA YA MAKAMPUNI 5284 YANAYOTARAJIWA KUFUTWA NA BRELA

Amesema kampuni hizo zitatangazwa katika magazeti na vyombo mbalimbali vya habari ili wamiliki waweze kujua kusudio hilo huku nakala ya barua itapelekwa katika anuani halisi za kampuni hizo

"Notisi hizi zitatolewa kwa awamu tatu, awamu mbili za kwanza zitakuwa siku 30 kila moja na ya tatu itakuwa siku 90 ili kutoa nafasi kwa wamiliki kuthibitisha kama kampuni zao zinafanya biashara," amesema.

Amesema notisi ya kwanza na pili itahusisha kampuni 5,284 zilizosajiliwa nchini na kampuni 392 zilizosajiliwa nje ya nchi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages