Breaking

Saturday 7 May 2022

DED MUSOMA VIJIJINI APEWA MIEZI MITATU KUJITATHMINI UTENDAJI WAKE WA KAZI





Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa ametoa miezi mitatu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Palela Nitu Msongela kujitathimini utendaji wake kwenye usimamizi wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Hospital ya Wilaya na Ujenzi wa jengo la Halmashauri.


Waziri Bashungwa ametoa uamuzi huo leo Jumamosi Mei 7, 2022 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Halmashauri na Hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.


Amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe kuunda timu ya uchaguzi ili kujiridhisha iwapo thamani ya fedha umezingatia katika ujenzi wa Miradi ya Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na Hospitali ya Wilaya inayojengwa katika kijiji cha Suguti, Mkoani Mara.


Amesema miradi mingi ya Halmashauri hiyo imekuwa ikidorora na kujengwa kwa kusuasua na kupelekea miradi mingi kutokukamilika kwa wakati.


"Ninamuagiza Katibu Mkuu kuhakikisha a aunda timu ambayo itachunguza matumizi ya fedha zilizotumika katika ujenzi wa miradi hiyo ili kuona dhamani ya fedha iliyotumika inaenda sambamba na ubora wa majengo yaliyojengwa“ amesema Bashungwa


Waziri Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Hapi kusimamia ujenzi wa miradi hiyo na kumtaka kutumia Kamati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vya Mkopo wa IMF kusimamia ujuzi wa Miradi hiyo.


Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe Ally Hapi amesema kuwa wataendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo na watumishi watakaobainika ni wabadhilifu katika miradi watachuliwa hatua za kiutumishi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages