Breaking

Wednesday 11 May 2022

ELON MUSK ATANGAZA KUIREJESHA AKAUNT YA TRUMP TWITTER


Na Said Muhibu


Tajiri mkubwa zaidi duniani Elon Musk ametangaza kuirejesha akaunti ya Twitter aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump iwapo dili lake la kupata kampuni hiyo litakamilika.


Kauli hiyo ameitoa Jumanne  Mei 10, 2022 katika mkutano wa Financial Times' Future of the car, na kusema kuwa uamuzi wa Twitter kuifungia akaunti ya Trump ulikuwa ni kosa.


"Nadhani haikuwa sahihi kuipiga marufuku akaunti ya Donald Trump, nadhani lilikuwa ni kosa," Musk alisema.


Akaunti ya Twitter ya Donald Trump ilizuiwa mnamo mwaka 2021 kufuatia mandamano ya januari 6 kwa kukiuka sheria za jukwaa dhidi ya uchochezi wa ghasia.


Hata hivyo Trump kwa upande wake amesema hatarejea kwenye Twitter hata kama akaunti yake itarejeshwa, badala yake ataendeleza ubia wake kwenye mitandao ya kijamii, Truth social ambao kufikia sasa unatatizika kujiondoa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages