Breaking

Thursday 26 May 2022

JAJI MKUU UGANDA ATEMBELEA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO

Jaji Mkuu wa Uganda, Alfonse Owinyi- Dollo akitoa salamu za ujumbe katika ziara yake
Viongozi walioambatana na Jaji Mkuu wa Uganda, Alfonse Owinyi- Dollo wakiwafuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa inaendelea katika kikazo kwenye wakati wa ziara hiyo.
Jaji Mkuu wa Uganda,Alfonse Owinyi- Dollo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Uganda.
Jaji Mkuu wa Uganda, Alfonse Owinyi- Dollo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa menejimenti ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto

**********
Na lango la habari

Jaji Mkuu wa Uganda, Mhe. Alfonse Chigamoy Owiny-Dollo amefanya ziara ya kutembelea Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na kujionea shughuli mbalimbali zinafanywa.

Katika ziara yake aliyoifanya 
Jumatano Mei 25, 2022 Jaji Owiny-Dollo ameambatana na Maafisa 12 kutoka nchini Uganda. 

 Miongoni mwa aliombatana nao ni Jaji Kiongozi wa Uganda Mhe. Dkt. Flavian Zeija, Msajili ya Mahakama ya Uganda, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa JTI Uganda, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya JTI Uganda, Msajili waTaasisi ya JTI Uganda na viongozi wa International Development Law Organization Uganda(IDLO).

Akizungumza wakati akiwa kwenye ziara hiyo, Jaji Owiny-Dollo alisema kuwa lengo la ziara yao ni kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa jinsi ya kuwandaa Maafisa Mahakama ambao wamepangiwa majukumu mapya na kujifunza jinsi ya kuijengea uwezo Taasisi ya Mafunzo ya Kimahakama ya nchini Uganda (JTI) pia kujenga ushirikiano katika masuala mbalimbali yanayohusu vyuo na jinsi ya kuiwezesha Mahakama ya Uganda kufanikisha katika maboresho yake kiutendaji.

Amesema kuwa mafunzo ya kuwandaa Maafisa wa Mahakama wanaopewa majukumu mapya ni muhimu katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo huduma bora ya utaoji haki kwa wananchi.

Ameongeza kuwa wanataka kupata uzoefu ambao utawasaidia yeye na ujumbe kutoka Chuo cha Mahakama cha Uganda kuwawezesha watumishi wanaopewa majukumu mapya kupata mafunzo ambayo yatasaidia katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

“Maafisa wa Mahakama walioandaliwa kwa kupewa mafunzo mazuri wataelewa vema majukumu yao na mambo ambayo anatakiwa kufanya katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kupata haki wanapokuwa na mashauri” amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Dkt. Gerald Ndika alionyesha furaha yake kwa kushuru ugeni huo na kusema kuwa ujio wao ni fursa muhimu ambapo wataitumia kwa kujifunza mambo mbalimbali na kubadilishana uzoefu jinsi vyuo vya Mahakama vinavyofanya kazi.

Naye Mkuu wa Chuo na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Dkt. Paul Kihwelo alielezea historia ya Chuo hicho ambacho kilianzishwa kwa Sheria ya Bunge, Sheria Namba 3 ya 1998 ambapo Kilianza kazi yake Oktoba 23, 2000 na kilikuwa kinatoa Cheti na Diploma ya Kozi za Sheria huku 
Uzinduzi rasmi ulifanywa na Rais Benjamin Mkapa tarehe 3 Agosti 2001. 

Pamoja na historia hiyo Mkuu wa Chuo alieleza lengo la madhumuni ya kuanzishwa kwa Chuo ilikuwa ni kujengea uwezo watumishi wa Mahakama.

Ziara hiyo ni sehemu ya ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Uganda na ujirani mwema kati ya nchi hizi mbili. 

Sambamba na kutembelea maeneo mbalimbali ya Chuo, Wageni hawa wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vilivyopo katika Wilaya ya Lushoto.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages