Na Said Muhibu,Lango la Habari
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wameingia kwenye orodha ya watu 100 bora wenye ushawishi zaidi duniani, orodha hiyo iliyotolewa jana Mei 23 na jarida la TIME limeorodhesha watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani kwa mwaka 2022.
Marais hao wameingia kwenye orodha hiyo kufuatia ushawishi walionao kama viongozi wa nchi kubwa barani ulaya, kila rais ana utashi wake katika kuiongoza nchi yake juu ya kufikia maendeleo ndani na nje ya nchi zao.
Marais hao wamekuwa kwenye mzozo wa muda mrefu tangu Urusi ivamie Ukraine mnamo Februari 24 mwaka huu na kusababisha maafa makubwa ikiwemo kupanda kwa bei za mafuta na vyakula duniani kwa ujumla.
Hata hivyo Viongozi mbalimbali na wasanii wametatajwa kwenye orodha hiyo akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, Kansela wa ujerumani Olaf Scholz na waigizaji wa filamu Zendaya na Simu Liu.