Breaking

Tuesday 24 May 2022

AJALI YA BUS YAUA WANNE NA KUJERUHI 30 - USHETU






WATU wanne wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa katika ajali ya Basi la Abiria kampuni ya RUKSA CLASS baada ya kupinduka katika Kijiji cha Kayenze Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga amesema ajali hiyo imetokea Jana Mei 23, 2022 imetokana na mwendokasi hali iliyompelekea dereva kushindwa kulimudu basi hilo kwenye kona.

Amesema waliofariki dunia ni wanaume watatu na mwanamke mmoja ambapo kati yao mmoja ni mwendesha baiskeli ambaye alikuwa pembezoni mwa barabara hivyo basi hilo lilimgonga na kupelekea kifo chake.


Kiswaga amesema Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni watu zaidi ya 30 ambapo wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kuondoka lakini waliosalia ni wanne wanaoendelea na matibabu na miili ya marehemu ipo katika hospitali ya Wilaya ya Kahama.

Aidha, amewapongeza wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kushiriki uokoaji katika ajali hiyo sambamba na kuhakikisha ulinzi wa mali za abiria huku akiwataka kutoa taarifa za mwendokasi ili kuzuia uvunjifu wa sheria za barabarani.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya Festo Kiswaga amewataka madereva wote kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali huku akisema madereva wote watakaobainika kukiuka sheria watakamatwa na kunyang’anywa leseni zao kwa mjibu wa sheria.





Source: GlobalPublisher
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages