Breaking

Tuesday 24 May 2022

MADIWANI WAMFUKUZA MGANGA MKUU KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAFUTA




Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro imemsimamisha kazi Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dustan Mshana kwa tuhuma ya wizi wa mafuta lita 100, kununua kumpyuta chakavu pamoja na kutosimamia vizuri idara yake hiyo.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Rachael Nyangasi, alisema hayo juzi kuwa mbali na huhuma hizo, pia Dk. Mshana anatuhumiwa kusimamia mapato lindwa ikiwa na matumizi mabaya ya ofisi kushindwa ni pamoja yake.

"Dk. Mshana anatuhumiwa kufoji saini za madereva na kuchukua mafuta lita 100 za magari ya halmashauri hii, lakini ameshindwa kutii maagizo ya mwajiri wake yaliyomtaka kuwasilisha kumpyuta mpya na sio chakavu," alisema Nyangasi.

Nyangasi alisema mwajiri alimtaka Dk. Mshana kununua kompyuta 19 mpya kwa ajili ya kukusanya mapato lindwa, lakini katika ukaguzi uliofanywa na mkaguzi wa ndani umebainika kuwa ni kumpyuta tatu pekee ndiyo mpya na nyingine ni chakavu.

Alisema Baraza la Madiwani limeona itoe uamuzi huo wa kumsimamisha Mganga Mkuu huyo ili iwe fundis aiokwa waadilifu huyo ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wa wilaya hiyo ya Gairo wasiokuwa waadilifu na amewataka watumishi kuwa na waledi.

Mwenyekiti huyo alisema katika ununuzi wa kompyuta hizo kuna watumishi wengine kadhaa nao wanatuhumiwa kuhusika na baraza limemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri kuchukua hatua stahiki kwa wahusika wote.

"Serikali imeongeza mishahara kwa wa tumishi wake, lakini bado kuna baadhi ya watumishi wasio waadilifu na kusababisha kutumia fedha zinatotolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo ya wana Gairo kwa matumizi yao binafsi, hili halikubariki," alisema.

Aidha, aliwataka madiwani wa halmashauri hiyo kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato kwenye kata zao na pia aliwahimiza kuhakikisha waziba mianya yote ya upotevu wa mapato kwa maslahi mapana ya maendeleo ya Gairo na taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabiri Makame, alisema wote waliohusika na hoja za Mkaguzi wa Fedha za Serikali (CAG), wachukuliwe hatua kali ili kitendo hicho kisiweze kujirudia tena upya katika wilaya yake hiyo.


Source; Nipashe
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages