Breaking

Friday 6 May 2022

SABAYA NA WENZAKE WAWILI WAACHIWA HURU




Mahakama Kuu imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada ya kubaini kulikuwa na mapungufu katika mwenendo mzima wa kesi, pamoja na kutofautiana kwa mashahidi.

Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Mbali na Sabaya, wengine ni Sylvester Nyegu na Daniel Mbura.

Hata hivyo, Sabaya ataendelea kukaa mahabusu kutokana na kukabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages