Breaking

Monday 16 May 2022

TUME YA MADINI YAWAPIGA MSASA WACHIMBAJI WADOGO MANYARA





Timu ya wataalam waandamizi wa Tume ya Madini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Mhandisi Henry Mditi wameendelea kutoa mafunzo kwa wamiliki wa migodi, wachimbaji wadogo wa madini na wasimamizi wa baruti.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatatu Mei 16, 2022 katika eneo la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara na kuzinduliwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba.


Mada zilizotolewa ni pamoja na usimamizi wa afya, usalama, baruti na sheria za madini na kanuni kuhusu eneo tengefu la Mererani na uchimbaji salama migodini.

Aidha, utunzaji wa mazingira migodini na usimamizi wa baruti migodini ulielezwa katika mafunzo hayo.


Wakizungumza katika nyakati tofauti wadau wa madini waliohudhuria mafunzo hayo wameipongeza Tume ya Madini kwa utoaji wa elimu safi na kushauri elimu kuendelea kutolewa kwenye maeneo mengine yenye shughuli za uchimbaji wa madini nchini.







Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages