Breaking

Saturday 14 May 2022

WAKANDARASI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA BRELA




Wakala wa Usajili wa Biashara na  Leseni (BRELA)  imewataka wakandarasi nchini kuendelea kutoa ushiriakiano kwa BRELA ili kuwezesha kazi zao kufanyika kwa ufanisi zaidi.


Hayo yamebainishwa Ijumaa Mei 13, 2022 na Afisa Usajili wa BRELA, Gabriel Girangay wakati wa mkutano wa wakandarasi katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.


Girangay amesema kuwa wakandarasi ni wadau muhimu hivyo wanapaswa kutoa ushirikiano wa karibu  kwani  kabla ya kwenda kusajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi wanatakiwa kusajili kwanza makampuni yao  BRELA.


Wakandarasi ni watu muhimu na inapaswa kuhakikisha mnahuisha taarifa zenu kwa wakati ili muweze kutambulika kwenye mfumo na iwasaidie kushindana katika zabuni mbalimbali zinazotangazwa.” amesema Girangay


Ameongeza kuwa, wakati wa kuhuisha taarifa za wanahisa  BRELA ni kiungo muhimu hivyo ni vyema kutoa ushirikiano wa kina  ili  kufanikisha shughuli zao za ukandarasi.


Pia amewasihi kuacha  kuwatumia "vishoka" ambao wanasababisha ucheleweshaji wa michakato wa urasimishaji wa biashara.


Ameeleza kuwa, mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao ( Online Registration System-ORS) unatoa nafasi kwa kampuni kupata huduma za BRELA mahali popote.


 Aidha ametoa wito kuhusu uwasilishaji wa taarifa za Wamiliki Manufaa kabla ya Juni 30, 2022 ili kukidhi takwa la kisheria.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages