Breaking

Friday 20 May 2022

WAZIRI BASHUNGWA ATAKA WAMACHINGA WAPEWE MIKOPO YA GHARAMA NAFUU




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa ametoa wito kwa Sekta za kifedha na Taasisi binafsi kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutoa huduma za mikopo ya gharama nafuu kwa ajili ya kukuza biashara za wajasiriamali wadogo.


Akifungua kongamano la Jukwaa la Maendeleo ya Sekta ya Fedha leo Mei 20, 2022 Jijini Dodoma Mhe. Bashungwa ameziomba taasisi  kuinua kundi hilo kwa lengo  kwa kutoa mikopo ili kuboresha mazingira ya biashara na kuinua wigo wa ulipaji kodi.


Bashungwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan  kwa dhamira ya kutambua Wamachinga  kuwa Sekta rasmi na kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara


Amewahakikishia wajasiriamali wadogo (wamachinga) wote nchini kuwa Serikali ina dhamira ya dhati katika kuhakikisha inatengeneza mazingira wezeshi kwa ajili yako kote nchini hivyo Wizara husika  zitahakikisha zinatekeleza kwa weledi dhamira ya Rais Samia ya kuleta maisha bora kwa machinga inafanikiwa.


Aidha, amewaagiza Makatibu wa  Wizara ya fedha, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsi, wazee na mahitaji Maalum  na Ofisi ya Rais TAMISEMI  kukaa kwa pamoja ili kujadili na kuchambua maazimio ya kongamano hilo na kupata muelekeo wa Sekta ya Machinga nchini


Bashungwa amesema Sekta ya Machinga ina fursa kubwa katika kuchangia uchumi wa nchi hivyo amewataka viongozi mbalimbali kuhakikisha wanatumia kongamano hilo kujadili kwa kina maeneo yaliyofanywa vizuri katika sekta hiyo, changamaoto zilizopo na fursa za kiuchumi ambazo zikisimamiawa ipasavyo zitaleta mafanikio katika sekta ya Machinga.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages