Breaking

Saturday 28 May 2022

WAZIRI MCHENGERWA AWAONGOZA WATANZANIA KUTAZAMA FAINALI UEFA - TANZANITE BRIDGE


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa usiku wa  leo majira ya saa nne usiku , Mei 28, 2022  amewaongoza mamia ya wapenzi wa soka nchini kutazama mbashara fainali za mashindano ya 67 ya UEFA baina ya Timu ya Real Madrid na Liverpool  kupitia DStv kwenye daraja jipya la Tanzanite jijini Dar es Salaam.


Mhe. Mchengerwa ameambatana na Katibu Mkuu, Dkt.  Hassan Abbasi na Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu na Watendaji kutoka  Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kabla ya mechi  hii yenye mvuto mkubwa  hapa nchini na duniani kote, Filamu ya Royal Tour imeoneshwa na  kuangaliwa na mamia ya wadau waliokuja kushuhudia tukio hili la kihistoria  kwenye sekta ya Michezo nchini.


Filamu hii iliyomshirikisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan ambayo imeifungua Tanzania duniani kwenye sekta mbalimbali imewavutia wapenzi wa soka waliokuja kutazama fainali hizo.

Waziri Mchengerwa amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuendelea  kutumia  sekta za michezo  na Sanaa kuitangaza Tanzania na vivutio  vyake  duniani kwa kuwa zimebeba idadi kubwa ya Tanzania  na kuongeza kuwa  sekta hizo ndiyo nguvu shawishi ya Serikali zinazowapa watanzania wengi zaidi furaha  na faraja.


Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Heineken Nchini ambayo ndiyo mdhamini mkuu  wa tukio hilo, Bi.Fatma Mnaro amesema kuwa lengo la kuonesha mubasha  fainali za UEFA hapa nchini  kupitia DSTv  ni kutaka kuwafanya  wapenzi wa soka walione shindano hilo kwa ubora wa hali ya juu kama ambavyo watakavyoshuhudia wale ambao watahudhuria mtanange huo nchini  Paris nchini Ufaransa.

Aidha,  Bi. Mnaro ameongeza kuwa pamoja na kurushwa mubashara  kwenye Daraja la Tanzanite  pia  kuna sehemu  mbalimbali  za majiji makubwa ambazo pia zinaonesha ambazo ni pamoja na The Cask jijini Mwanza, City Pub jijini Mbeya, Arusha na Capetown Fish Market, Samaki samaki na Triple 777 jijini Dar es Salaam.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages