Na Ayoub Julius, Lango la habari
Mabingwa wa kihistoria nchini Tanzania Young Africans wametangaza kuachana na Kiungo Mshambuliaji raia wa Burundi Saido Ntibazonkiza
Yanga wametoa taarifa hiyo mapema leo wakieleza kuwa Saido amemaliza mkataba wake wa kuitumikia Yanga leo tarehe 30 Mwezi Juni 2022 alioutumikia kwa muda wa miaka miwili.
Aidha Klabu ya Yanga imemtakia kila la kheri Mchezaji huyo katika maisha yake ya soka huko atapoelekea baada ya kuwa amemalizana na Yanga.
Kiungo huyo mwenye Umri wa Miaka 35 amefanikiwa kucheza michezo 19 kapachika bao 7 na ametoa pasi za magoli 4 mpaka sasa katika ligi kuu ya Tanzania Bara NBC Premier League
Yanga wamebakiza michezo minne(4) pekee ili kukamilisha mzunguko wa pili wakiwa na alama 64 mbele ya mahasimu wao Simba sc wenye alama 51 wakiwa na michezo mitano(5) ikiwa imesalia.