Breaking

Monday 20 June 2022

BALOZI POLEPOLE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ZIMBABWE NCHINI MALAWI




Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Humphrey Polepole amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Zimbambwe nchini Malawi na Amidi wa Mabalozi wa Nchi za Afrika Dkt. Nancy Saungweme.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Jumatatu Juni 20, 2022 Balozi Polepole ametumia nafasi hiyo kumhakikishia ushirikiano katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kidiplomasia baina ya Jamhuri ya Muungano ya Muungano wa Tanzania na Nchi ya Zimbabwe.

Kwa upande wake Balozi Saungweme amesema kuwa kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mojawapo ya nchi marafiki wa Zimbambwe tangu harakati za ukombozi hata sasa na akatumia nafasi hiyo kuishukuru Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kupigania haki za Wazimbabwe na kwa umahususi katika kampeni ya kuiondolea vikwazo vya kiuchumi mara moja Nchi ya Zimbabwe.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages