Breaking

Friday 17 June 2022

GENERALI MABEYO AIAGA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MWANZA




Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel amemshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Generali Venancy Mabeyo kwa Utumishi wake Mema kwa wananchi wa Mwanza na amemtakia Afya njema wakati wote hata baada ya Utumishi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza imeeleza kuwa Rc Gabriel amebainisha hayo leo Juni 17, 2022 wakati Jenerali Venancy Mabeyo alipofika kushukuru na kuwaaga wananchi wa Mwanza katika kuelekea kustaafu kwake kwa Utumishi ndani ya Jeshi hilo hapo mwezi Julai 2022.

"Wananchi wa Mwanza wanakukumbuka sana kwa namna ulivyoshrikiki wewe binafsi kwenye Operesheni ya Uokoaji iliyokua na ufanisi mkubwa iliyofanyika baada ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere tarehe 20 Septemba 2018 katika kata ya Bwisya Kisiwani Ukara-Ukerewe Mkoani Mwanza". Amesema Mkuu wa Mkoa.



"Ndugu Mkuu wa Majeshi, WanaMwanza tumeridhika na tunashukuru kwa utumishi wako na tunamuomba mwenyezi Mungu akuangazie mwanga mwingine kwenye maisha yako yote" Mhe Gabriel.

Kwa upande wake Jenerali Mabeyo amesema amefika Kanda ya ziwa kuwasalimia na kuwaaga rasmi kwani anafikia mwisho wa Utumishi kwenye Jeshi alilojiunga tangu 1979.

"Kwangu ni faraja kubwa kwamba nimeishi katika nafasi na maeneo mbalimbali, nimejenga familia kama mtumishi ndani ya jeshi na nje ya jeshi na karibu watanania wote nimeishi nao katika misingi ya kulinda mipaka ya nchi na mali zao." Amebainisha.

"Nafarijika mno kwamba mmenipa nafasi nije niwaage, kanda ya ziwa ndio nyumbani na wengi wangependa wanione na sasa nimekamilisha mzunguko wa Machweo na Mawio na sasa jua linazama kwenye maisha ya kijeshi ambayo nimekaa kwa muda mrefu." Mkuu wa Majeshi


Aidha, Jenerali Mabeyo amewaasa vyombo vya ulinzi na watumishi kuendelea kushirikiana na ametumia wasaa huo kuwashukuru huku akibainisha kuwa wamemlea na kumuwezeaha kufanya kazi kwa utulivu.

"Nitarudi kijijini nilikozaliwa lakini nitakua na fursa za kuzunguka hapa na pale ili nishirikiane na wananchi wenzangu na kwakweli navishukuru sana vyombe vingine vya ulinzi na usalama kwani wamenipa ushirikiano mkubwa sana na ndio maana afya yangu bado ni nzuri kutokana na utulivu na ushirikiano." amesema.

Mwisho

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages