Breaking

Thursday 23 June 2022

RAIS SAMIA ATOA MAAGIZO MAZITO AJALI YA TRENI TABORA



Na Samir Salum, Lango la habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza kufanyika uchunguzi na kubaini chanzo cha tukio la treni ya abiria kuanguka na kusababisha vifo vya watu kadhaa eneo la Malolo Mkoani Tabora.

Rais samia ametoa agizo hilo leo Alhamisi Juni 23, 2022 ambapo ametuma salamu za rambirambi kwa wafiwa kutokana na watu wanne kufariki katika ajali hiyo.

“Nawapa pole wafiwa, nawaombea marehemu wapumzike kwa amani na majeruhi wapone haraka. Nimeagiza tuliowapa dhamana ya eneo hili kufuatilia na kubaini chanzo, na kuchukua hatua stahiki,” – Rais Samia.


Ajali hiyo ilitokea jana Juni 22, 2022 ambapo baadaye Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema kulikuwa na hujuma baada ya kukuta kipande cha reli kiliondolewa na kisha kurudishwa kwa kuegeshwa katika eneo la ajali.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages