Breaking

Monday 20 June 2022

TAARIFA MUHIMU KWA WAFANYABIASHA WA MAHINDI KUTOKA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI


Ubalozi wa Tanzania Nchini Malawi umesema kuwa Serikali ya Malawi imesitisha kuuzwa kwa Mahindi nje ya nchi kutokana na mashaka ya kuwa na upungufu wa chakula.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu Juni 20,2022 na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Humphrey Polepole kwenda kwa wafanyabiashara wa mazao ya wa Tanzania.

Balozi Polepole amesema Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi unafuatilia suala hili kwa karibu huku ukiwataka Wafanyabiashara kusitisha mpango wa kununua mahindi nchini malawi mpaka Ubalozi utakapotoa taarifa nyingine.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages