Breaking

Monday 27 June 2022

TAMASHA KUBWA LA UTAMADUNI KUFANYIKA KITAIFA DAR, KUANZA JULAI MOSI, 2022


Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo imeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan la kufanya Tamasha kubwa la kitaifa la Utamaduni ambalo linakwenda  kushirikisha zaidi ya wadau elfu ishirini.


Akizungumza kwenye kikao cha maandalizi cha pamoja baina ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amesema tamasha hilo la kihistoria linajumuisha mikoa yote ya Tanzania linatarajia kuanza Julai Mosi mwaka huu  katika uwanja wa Uhuru ambapo  maonesho mbalimbali ya  vyakula na ngoma za asili.


Amefafanua kwamba Julai, 2, 2022  kutakuwa na matembezi  maalum ya kuzunguka jiji la Dar es Salaam kwenye madaraja yote  ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kasssim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. 


Kwa upande mwingine, Yakubu amesema siku ya  Julai 3, 2022 itakuwa siku maalum  ya miondoko ya taarabu utakaofanyika eneo la ufukwe wa  Coco  pembezoni  mwa  Bahari ya Hindi ambapo Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Tulia Ackson  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.


Amesema tamasha hilo pia litapambwa  na  vikundi  mbalimbali  maarufu vya taarabu  kutoka ndani na nje ya nchi ambapo amesema  vikundi vitano vinatoka Zanzibar, vikundi vingine  vitano  kutoka  Tanzania  bara  huku  vikundi vingine  vikitokea Comoro, Burundi na Mombasa nchini Kenya. 


Amevitaja vikundi kutoka Zanzibar kuwa ni pamoja na zahati zamani, Nadikhwan safaa, wapendanao modern culture, kikundi cha culture, chama cha wasanii wa muziki Zanzibar.


 Kwa upande wa Tanzania bara ni pamoja na Jahazi modern taarab, First Class, Wana nakshinakshi, Bablom na East Africa Melody na  wasanii   binafsi maarufu  pia wamealikwa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages