Breaking

Saturday 18 June 2022

TIMU YA KRIKETI YA WANAWAKE TANZANIA YATWAA UBINGWA KWIBUKA CUP RWANDA


Timu ya Tanzania ya  Wanawake ya Kriketi imetwaa Ubingwa kwenye mashindano ya Kwibuka Cup yaliyofanyika Nchini Rwanda.


Timu hiyo imechukua ubingwa wa bila kufungwa na timu yoyote kwenye Mashindano hayo ambayo yameshirikisha nchi nane ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana , Nigeria, Brazil na Ujerumani. 


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa ametoa pongezi kwa Timu hiyo kuchukua ubingwa huo.


Aidha amempongeza Raiz Samia kwa mchango wake mkubwa anaoutoa katika michezo.


Amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha michezo kwa kuweka mikakati  kabambe chini ya uongozi wa Samia imeleta matokeo chanya kwenye sekta za michezo na sanaa hapa nchini.


Amesema taarifa ya hali ya uchumi wa nchi iliyosomwa bungeni hivi karibuni imeonesha kuwa sanaa na burudani zimechangia kwa asilimia 19.4 katika kipindi cha mwaka 2021 na kuziacha kwa  mbali sekta mbalimbali.


Amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuifanya michezo kuwa uchumi badala mazoe ya kuifanya michezo kama  kitu cha burudani pekee.


Aidha, amesema Serikali tayari inazigharimia timu zote za taifa zinazojiandaa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa kwa kuziweka kambini kuanzia mwanzo wa mwaka huu.


Hivi karibuni Waziri Mchengerwa amekaririwa vyombo vya habari akisisitiza kuwa michezo na sanaa ni uchumi  hivyo wanamichezo na wasanii wanapaswa kutambua kuwa vipaji walivyonavyo ni mtaji wa maisha yao.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages