Breaking

Thursday 23 June 2022

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUACHA KUFANYA BIASHARA KWA MAZOEA

 

Wanawake wajasiriamali nchini wametakiwa kuacha kufanya biashara kwa mazoea badala yake kurasimisha biashara zao ili kupata fursa mbalimbali za kibiashara.

 

Wito huo umetolewa  tarehe 22 Juni, 2022 na Afisa Sheria kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Vicensia Fuko  wakati akitoa mada kuhusu huduma zinazo tolewa na Wakala katika Mafunzo ya  wanawake wajasiriamali kutoka mikoa  ya Tanzania Bara na Visiwani, yanayofanyika katika ukumbi wa JKT Mgulani Temeke, Jijini Dar es Salaam.


Bi. Fuko amesema wanaporasimisha biashara zao inawapa fursa mbalimbali  za kibiashara ikiwa ni pamoja na kupata mikopo kutoka taasisi za fedha na kushinda zabuni. 


"Nichukue fursa hii kuwahamasisha wanawake  wajasiriamali kuhakikisha kuwa mnarasimisha biashara zenu kupitia BRELA  na kwa sasa usajili unafanyika kwa njia ya  mtandao, hivyo hakuna haja ya kufika katika ofisi za BRELA, " amefafanua Bi. Fuko.


  Katika mafunzo hayo ya siku nne, washiriki watajadili masuala mbalimbali yatakayowawezesha kujikwamua kiuchumi sambamba na kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya

 kuanzishwa kwa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, ambao  mwanzilishi wake ni  Mama Anna Mkapa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages