Breaking

Tuesday 14 June 2022

WAZIRI MCHENGERWA AFANYA MAZUNGUMZO NA NGULI WA FILAMU NIGERIA


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana na msanii nguli kutoka Nigeria Jim  Iyke na kufanya mazungumzo ya mashirikiano katika kuandaa filamu za kimkakati za pamoja baina ya Tanzania na Nigeria 


Mazungumzo haya yamefanyika leo Juni 14, 2022 jijini Dodoma  ambapo wamekubaliana  kuwa na mashirikiano  kwenye filamu za kimkakati kwa faida za pande zote mbili.


Waziri Mchengerwa amesema mashirikiano hayo yataifanya Tanzania kunufaika zaidi kwa kufanya kazi na manguli wa filamu wa Nigeria ambao wanawapenzi  wengi duniani.

 Ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau mbalimbali duniani kuja kuwekeza  kwenye sekta ya Sanaa na Michezo.


Ameongeza kuwa kwa sasa  tayari imeshusha kodi ya zuio katika biashara ya filamu kutoka asilimia 15 hadi 10 ili kuyapa unafuu makampuni yanayofanya masuala ya filamu nchini.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages