Breaking

Monday 13 June 2022

WIZARA YA MADINI KUSHIRIKI MAONESHO MAKUBWA YA MADINI CANADA, DKT. BITEKO KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI


Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Canada  imeanza maandalizi ya kushiriki katika Maonesho Makubwa ya Madini yanayohusisha Wazalishaji na Watumiaji wa Bidhaa zinazohusisha Madini  Duniani ( PDAC), yanayotarajiwa kufanyika nchini humo.

Ujumbe wa Tanzania katika Maonesho hayo unahusisha Wizara ya Madini na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ambapo  wizara inatarajiwa kunadi fursa zake za kiuwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini kwa wawekezaji duniani.

Kwa mara ya kwanza Bara la Afrika limepewa kipaumbele kutangaza fursa zake za kiuwekezaji katika maonesho hayo.

Aidha, pamoja na kuonesha fursa hizo,  Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kutoa  mada kuhusu fursa za uwekezaji zilipo kwenye Sekta ya Madini  katika eneo la utafutaji madini ya aina mbalimbali, uchimbaji , uchenjuaji, biashara ya Madini pamoja na shughuli za kutoa huduma kwenye migodi ya Tanzania.

Hatua hiyo inalenga kuongeza uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Madini.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages