Breaking

Wednesday 20 July 2022

AJALI YAJERUHI WATU WANNE MOROGORO





Watu wanne wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Mkambalani wilayani Morogoro, ikihusisha basi la Happy Nation lenye namba za usajili T 702 DGF likilokuwa linatokea Dar es Salaam kuelekea Bukoba na lori la mizigo lililokuwa linatoka Zambia kwenda Dar es Salaam.

Ajali hiyo imetokea leo Julai 20, 2022, majira ya saa 3:00 asuhubi, ambapo baadhi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo wamesema kuwa kilichosababisha ni kutozingatiwa kwa sheria za barabarani wakiomba jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuongeza umakini ili kupunguza ajali zisizo za lazima.

Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Morogoro ACP Ralph Meela, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo chanzo cha ajali kinadaiwa kuwa ni uzembe wa dereva wa basi hilo Hassan Abdallah ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari lingine bila kuchukua tahadjari na kusababisha ajali hiyo.


Chanzo - EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages