Breaking

Friday 8 July 2022

DKT. KIRUSWA ATAKA USALAMA MAHALA PA KAZI IWE KIPAUMBELE MIGODINI




Imeelezwa kuwa, usalama mahala pa kazi ni jambo muhimu ambalo linapaswa kuzingatiwa na wachimbaji wote wa madini nchini akiwemo mwajiri pamoja na waajiriwa, wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa.

Hayo, ameyabainishwa na Dkt. Kiruswa baada ya kutembelea mgodi wa uchimbaji na uchenjuaji madini ya dhahabu wa Maweni Gold Mine uliopo katika kijiji cha Maweni mkoani Manyara.

Dkt. Kiruswa amesema usalama katika shughuli za uchimbaji madini ni suala muhimu kuliko hata madini yanayochimbwa katika eneo husika ambapo amewataka waajiri na waajiriwa kuhakikisha kila mmoja kwa nafasi yake anajilinda na kuwalinda wengine.

Sambamba na hayo, Dkt. Kiruswa amewapongeza wawekezaji katika mgodi huo na kuwataka kuzingatia Sheria za Madini ikiwemo kulipa kodi na tozo mbalimbali za serikali.

Naye, Kamshna wa Madini Dkt. Abdulrahiman Mwanga amemtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Manyara Mhandisi Ernest Sanka kutoa semina na mafunzo mbalimbali kuhusu elimu ya usalama mahala pa kazi ili wafanye shughuli zao kwa usalama.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwanga ameutaka uongozi wa kampuni ya Maweni Gold mine Ltd kuhakikisha unajenga mahusiano mazuri na jamii iyozunguka eneo wanalofanyia shughuli zao.

Naye, Meneja wa Maweni Gold Mine Ltd Emmanueli Maguzu amesema mgodi wao umefunguliwa rasmi tarehe 4 Julai na unatarajiwa kuzalisha kilo moja na nusu za dhahabu kwa mwezi.

Pia, Maguzu amesema kuwa, kwa sasa mgodi huo umeajiri wafanyakazi 20 upande wa uchenjuaji, wapishi wawili pamoja na walinzi 10 ambapo wanategemea kuajiri wafanyakazi wengi zaidi watakapoanza shughuli za uchimbaji ambapo kwa sasa wameanza shughuli za uchenjuaji pekee.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages