Breaking

Sunday, 17 July 2022

KIONGOZI MBIO ZA MWENGE ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIRADI UKEREWEKiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, 2022, Sahili Geraruma, ameonesha kuridhishwa na Ujenzi wa Mradi wa Kituo cha afya Igalla kilichopo Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza unatekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 402.3

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza imeeleza kuwa Geraruma ametoa kauli yake leo Julai 16 baada ya kukagua mradi huo ambapo kabla hajaweka jiwe la msingi amesema kwa jinsi ambavyo umetekelezwa hadi hatua ya sasa inadhihirisha kwamba ukikamilika thamani halisi ya fedha itaonekana wala hakuna mashaka yoyote juu ya utekelezaji wa mradi huo.

Amesema hali hiyo inaashiria kwamba kila mtumishi aliwajibika na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa mradi huo ambao ulioanza kutekelezwa Januari 31, 2022 unatarajiwa kukamilika Julai , 30, mwaka huu.

“Mwenge wa Uhuru hakika umeridhishwa kabisa bila mashaka yoyote na matumizi ya fedha katika kuutekelezamradi huu maana ni mzuri sana na kila ambacho kiko kwenye ramani mmefuata tena kwa ubora pongezi kubwa kwa halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.

“Ufanisi kwenye mradi huu umeonekana kutokana na usimamizi mzuri ulioufanya Mkurugenzi wa Halmashauri hii Emmanuel Sherembi nami nakuombea kwa Mungu ukamilishe mradi huu kwa wakati,”amesema na kuongeza

“Mtu akifanya jambo zuri msifie na akikosea mkosoe na umchukulie hatua, narudia tena hakika Mwenge wa Uhuru umeridhishwa sana na utekelezaji wa mradi huu ambao ukikamilika utawapunguzia wananchi wa eneo hili umbali wa kufuata huduma za afya zilizoboreshwa hilo ndiyo lengo la serikali kwa wananchi wake, mapendekezo zingatieni muda katika kuukamilisha, viwango na ubora,’amesema Geraruma.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo kwa kiongozi huyo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Dkt.Getere Nyangi, amesema kiasi cha Shilingi milioni 400 katika kuutekeleza inatokana na makusanyo ya mapato ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022 , Shilingi 870,000/= michango ya wananchi na Shilingi milioni 1.5 fedha ya michango ya mwenge wa uhuru mwaka huu.

“Katika mradi huu tutajenga jengo la wagonjwa wa nje, maabara, upasuaji, kulaza wagonjwa na kuhifadhia maiti, ukikamilika utaboresha huduma za tiba na kinga.

Source: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza 

Pages