Breaking

Saturday 30 July 2022

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KULAWITI MTOTO WA MIAKA MITANO



Mahakama ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe imemuhukumu kifungo cha maisha James Uhaula (65) Mkazi wa Kijiji cha Amani kwa kosa la kumlawiti Mtoto wa miaka mitano.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ludewa, Isaac Ayengo amesema Mtuhumiwa alitenda kosa hilo January 23, 2022 nyumbani kwake ambapo Mama wa Mtoto huyo Lucy Mkinga (23) alikuwa kanisani pamoja na Mtoto huyo na alipoona anaanza kusinzia akamwambia aelekee nyumbani akapumzike.

Amesema wakati Mtoto akielekea nyumbani Mtuhumiwa ambaye ni jirani yake alimuita ndani na kumpa pipi pamoja na simu ndogo aliyomuwekea mziki asikilize kisha akampakata na kumvua nguo kisha kumuingilia kinyume na maumbile.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mama wa Mtoto anasena aliporudi kanisani hakumkuta Mtoto nyumbani hivyo akaanza kumtafuta ndipo akasikia sauti ya Mwanae akilia kutokea katika chumba cha jirani yake ambaye ni Mtuhumiwa.

Aidha Mshtakiwa aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu kwakuwa anafamilia inayomtegemea na watoto watatu walio chini ya miaka 18, hata hivyo Hakimu Ayengo alitupilia mbali ombi hilo na kumpa hukumu ya kifungo cha maisha jela.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages