Breaking

Saturday 30 July 2022

WAZIRI BASHUNGWA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA MIKOA, AWAPA MIEZI MITATU KUKAMILISHA



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ametoa miezi mitatu kwa wakuu wa mikoa yote nchini kukamilisha miundombinu ya shule mpya zinazojengwa kupitia Mpango wa Kuboresha Elimu ya Sekondari(SEQUIP).

Programu hiyo inajenga shule mpya 214 katika kata za majimbo yote nchini ambazo hazina shule za sekondari au ambazo zinafunzi ambapo kila kata imepelekewa Sh milioni 470 huku ikipanga kutoa Sh milioni 130 kwa ajili ya miundombinu ya shule hizo

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa shule mbili za sekondari wilayani Kiteto, Bashungwa alisema wakuu wa mikoa wanapaswa kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo na kusisitiza kuwa Serikali haitatoa fedha zingine.

" Wakuu wa mikoa ama halmashauri muangalie ni namna gani mtakamilisha maeneo ambayo hayajakamilika, mahali pengine ndani ya nchi tumepeleka shilingi milioni 470 miondombinu yote imekamilika na imeanza kutoa huduma kwa watoto wetu."

" Nisisitize hatutaleta fedha ya ziada ya shilingi milioni 470 ambazo zimeletwa, hivyo wakuu wa mikoa wote nchini mfuatilie na mhakikishe miradi ya ujenzi wa shule mpya ambayo Serikali imepeleka muikamilishe ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa hadi mwishoni mwa Okotoba."

Bashungwa Pia amewaelekza wakuu wa mikoa kuhakikisha ifikapo Januari 2023 watoto wanaaza kusoma katika shule hizo mpya.

Kuhusu shule za sekondari zilizojengwa katika Kata ya Matui na Namelock, Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere kutumia vyombo vyake kufanya ukaguzi wa fedha zilizotumika katika shule hizo.

" Namemuelekeza Mkuu wa Mkoa Mzee na timu yako hebu jiridhishe na gharama halisi ambayo imetimika mahali hapa, kiasi ambacho mmekiomba hakitatoka Serikali kuu."

Katika shule ya Matui, ujenzi wa shule umefikia asilimia 85 na kuwa fedha zote Sh milioni 470 zimeisha hivyo kuhitaji Sh milioni 150 ili kukamilisha shule hiyo.

" Maombi ya nyongeza za fedha ni nyingi sana, hivyo kaeni muangalie kutumia vyanzo vya ndani kukamilisha, angalieni thamani ya fedha na kama kuna ubadhilifu Mkuu wa Mkoa chukua hatua."

Bashungwa pia amewataka wakuu wa mikoa na wakuu wa Wilaya kote nchini kusimamia sera ya elimu bila ada katika maeneo yao na kusisitiza kupiga marufuku na kukomesha michango holelaholela ambayo ipo nje ya miongozo ya Serikali.

"Tumashukuru Rais wetu kuendelea kutekeleza elimu bila ada na ni maelekezo ya Rais wetu kuwa wazazi na walezi hawasumbuliwi na michango holelaholela. Hivyo niwaelekeze wakuu wa mikoa na Halmashauri kusimamia sera ya elimu bila ada, michango holelaholela ambayo ipo nje ya miongozo ya Serikali."




Alisema pia sio maelekezo ya Rais Samia na Serikali kuwa wajawazito na watoto chini ya miaka 5 kutotozwa malipo wakati wa kupata matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kuwataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kusimamia maelekezo.

Naye Mbunge wa Kiteto, Edward Olelekaita alimshukuru Rais Samia kwa kuwezesha miundombinu kwenye sekta ya elimu, afya na barabara.

Alisema Wilaya ya Kiteto imejengwa shule za sekondari katika kata mbili huku kata nne zikikosa kabisa shule na kuiomba Serikali kuwapatia watumishi katika sekta ya elimu na afya.




(Mwisho).
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages