Breaking

Friday 29 July 2022

WAZIRI MKUU ATOA UFAFANUZI NYONGEZA YA MISHAHARA



WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali inapopandisha mishahara inaangalia zaidi kima cha chini na kwamba asilimia 23 iliyosemwa na Rais Samia Suluhu siku ya Mei Mosi iliwalenga zaidi wenye kima cha chini na sio wenye mishahara mikubwa.

Majaliwa ametoa ufafanuzi huo leo Ijumaa Julai 29, 2022 wakati akitoa tamko la Serikali Juu ya Nyongeza ya Mishahara.

"Tunaposema tunapandisha mishahara kima cha chini, maana yake wanaangaliwa sana wale wafanyakazi wa kipato cha chini, ile asilimia inayotamkwa inawalenga zaidi wale wa kima cha chini,"

“Asilimia 23 iliyotamkwa haijalipwa kwa watumishi wote, fomula iliyotamkwa si wote mpaka wenye mishahara mikubwa, walionufaika ni wenye mishahara midogo.-Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ufafanuzi nyongeza ya mishahara.”


“Hao wanaosema tumeongeza sh 20 ni wenye mishahara mikubwa, wako kwenye asilimia 22, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mameneja, Wakurugenzi na Wakuu wa Mikoa ambao kidogo wana mshahara unaotosha” Mhe. Majaliwa, akifafanua nyongeza ya mishahara.


"Ukiangalia mshahara kama wa Waziri wamepata 0.7%, sasa nani amepata hiyo ni yule mwenye kipato kikubwa, ujumbe wa msingi ni kwamba asilimia 23 iliyotamkwa haijalipa watu wote,"


“Upandishaji wa mishahara tunaangalia pia hali ya uchumi nchini, tusikwame kufanya mambo mengine tunajua watendaji wenyewe ndiyo sisi, lakini pia tunaangalia gurudumu hili tunavyolipeleka tusije tukalikimbiza likatukwamisha,” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages