Breaking

Friday 29 July 2022

WATU 42 WAFARIKI KWA KUNYWA POMBE YA METHANOL




Takriban watu 42 wamefariki na wengine 100 wamelazwa Hospitalini magharibi mwa India baada ya kunywa pombe ya Methanoli huku Polisi wakitangaza msako mkali kwa wafanyabiashara wa pombe nchini nzima wanaodaiwa kuuza pombe hiyo.

Mapema wiki hii idadi kubwa ya Watu wameripotiwa kuugua kwa kunywa pombe ya Methanol ambayo Watu hupendelea kunywa wakati wa baridi huku ikiuzwa mara nyingi katika maeneo ya vijijini hususan katika jimbo la Gujarat, Jimbo la Gujarat ni moja ya majimbo kadhaa nchini India ambapo unywaji na uuzaji wa vileo ni kinyume cha sheria.

Mnamo mwaka 2019, zaidi ya Watu 150 walifariki nchini India katika tukio kama hilo kaskazini mashariki mwa jimbo la Assam huku wengi wao wakiwa ni Wafanyakazi wa mashamba ya chai.

Mamia ya Watu hufariki kila mwaka nchini India kutokana na unywaji wa pombe za bei nafuu zinayotengenezwa kwenye viwanda vya kutengeneza pombe ambapo hivi sasa Mamlaka nchini humo imevamia maduka yote ya pombe kukagua vinywaji haramu ambavyo havijathibitishwa kwa matumizi ya Binadamu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages