Breaking

Wednesday 20 July 2022

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI DSFA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Emmanuel Andrew Sweke kuwa Mkurugenzı Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority - DSFA).

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Dkt. Sweke anachukua nafasi ya Bw. Zahor Kassim El-Kharousy ambaye amemaliza kipindi chake.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Sweke alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).

Taarifa imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza leo Julai 20, 2022.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages