Breaking

Thursday 28 July 2022

RAIS SAMIA ATEUA WAKUU WA MIKOA WAPYA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, amemhamisha kituo cha kazi aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Cuthbert Sendiga na kumpeleka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Pia, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Albert John Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, amemhamisha kituo cha kazi aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony John Mtaka na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Halima Omari Dendego, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Katika uteuzi huo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Nurdin Hassan Babu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Babu alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha.

Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt.Raphael Masunga Chegeni, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Pia Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Peter Joseph Serukamba, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

TAZAMA HAPA CHINI








Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages