Breaking

Saturday 23 July 2022

UNESCO YAKABIDHI SERIKALI NAKALA 800 ZA MADAFTARI YA KUSAJILI TAARIFA ZA UKATILI WA KIJINSIA ELIMU YA JUU

Muwakilishi wa Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, Bw. Mathias Luhanya akimkabidhi Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Amon Mpanju nakala za madaftari ya kusajili taarifa za ukatili wa kijinsia katika uzinduzi wa dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha Dodoma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Amon Mpanju akipokea nakala za madaftari ya kusajili taarifa za ukatili wa kijinsia katika uzinduzi wa dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha DodomaKutoka kushoto, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Faustine Bee, Muwakilishi wa mkuu wa ofisi ya UNESCO Bw. Mathias Luhanya,Mgeni rasmi Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe, Dr. Lilian Makalanga, mratibu wa kitengo cha Jinsia Chuo kikuu cha Dodoma, kwa pamoja wakikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa dawati.

**********************

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, kupitia programu yake ya “Our rights, Our Lives, Our future Plus” inayofahamika kama O3 Plus imeikabidhi Serikali nakala 800 za madaftari ya kusajili taarifa za ukatili wa kijinsia.

UNESCO imekabidhi madaftari hayo kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi maalum katika uzinduzi wa dawati la jinsia la chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Julai 23, 2022.


Lengo la kukabidhi madaftari hayo ni kusajili na kutunza kumbukumbu za taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyotolewa katika Dawati la Jinsia chuoni hapo.

Kwa kupitia mradi wa O3 Plus unaofadhiliwa na serikali ya Sweden UNESCO imechapisha nakala hizo za madaftari ya kusajili ikiwa na lengo la kuwezesha ufuatiliaji wa mwenendo wa shauri lililopewa rufaa, Kusaidia kuongeza wigo wa kupata taarifa za vitendo vya ukatili.

Pia Kuwezesha uandaaji wa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia zilizoripotiwa katika Dawati.

Aidha UNESCO inalenga kuongeza uelewa wa wadau zaidi ya 50,000 wa vyuo vikuu kuhusu ukatili wa kijinsia na vitendo vya unyanyasaji wa kingono, kutoa samani za ofisi kwa ofisi za madawati 10 ya jinsia ya vyuo vikuu, kutoa mafunzo kwa waratibu wa madawati ya jinsia wapatao 200 kutoka vyuo vikuu 15, na kuwezesha usambazaji wa nakala za vitabu vya rejista ya dawati la jinsia kwa mradi wote wa vyuo vikuu nufaika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages