Breaking

Friday 1 July 2022

WAANDISHI WA HABARI KARAGWE WATOA MSAADA NA ELIMU YA SENSA KWA WAFUNGWA GEREZA LA KAYANGA

Na Lydia Lugakila, Lango la habari


Waandishi wa habari wilayani Karagwe Mkoani Kagera kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo Bi Julieth Binyura wametembelea gereza la wafungwa la Kayanga na kutoa msaada wa vitu mbalimbali pamoja na elimu ya sensa ya watu na makazi,itakayofanyika Augost 23 ,2022.

Akizungumza katika eneo la Magereza hiyo walilotembelea Juni 30, 2022 Mwenyekiti wa wa klabu ya waandishi wa habari Mkoani Kagera Mwalimu Mbeki Mbeki amesema kuwa wameamua kuwatembelea wafungwa hao ili kuhamasisha elimu ya sensa ya watu na makazi.

Mbeki amesema kuwa sensa ni suala muhimu kwa ajili ya kuleta maendeleo katika Taifa hvyo ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha anahesabiwa.

Waandishi hao wametoa Msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo sukari,taulo za kike,mafuta ya kujipakaa,sabuni,miswaki ,na dawa ya meno vyenye thamani ya shilingi 250,000.

Aidha wana habari hao kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo wameandaa tukio la aina yake la usiku wa wana habari ,na wadau wa habari litakalofanyika leo Julai Mosi, 2022 katika ukumbi wa ELCT uliopo mjini kayanga ikiwa na lengo la kuhamasisha Elimu ya Sensa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages