Breaking

Friday 1 July 2022

MTUMISHI WA TANESCO AFARIKI AKIWA GESTI NA MWANAMKE



Mtumishi wa Shirika la Umeme (TANESCO) anayefahamika kwa jina la Yahaya Abdul, mkazi wa Manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi, amekutwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni alikoenda kujipumzisha na rafiki yake wa kike.

Tukio hilo limetokea mtaa wa Ikulu, Kata ya Kawajense, Mjumbe wa serikali ya mtaa huo George Kadesi, amesema baada ya kuona umati wa watu ukiwa umezungunguka gesti hiyo na alipofika alielezwa kuwa marehemu aliingia kwenye nyumba hiyo akiwa na rafiki yake wa kike.

Kwa upande wake mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ameeleza kuwa marehemu alifika majira ya saa 7:00 mchana na mpenzi wake lakini ameshangazwa kuona pikipiki ya mtu huyo mpaka asubuhi ikiwa pale gesti.

Kwa upande wake afisa uhusiano wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Katavi Emmanuel Tinda, amekiri kupokelewa kwa mwili wa mtu ambaye jina lake halijafahamika na uchunguzi wa kitabibu ili kubaini kifo chake unaendelea.

Aidha mwanamke huyo ambaye alikuwa naye gesti anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo.


Source: EATV

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages