Breaking

Thursday 14 July 2022

WANNE WATUHUMIWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA CHUO KIGOMA, WATATU WAKAMATWA




Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma kwa tuhuma za kumbaka Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 19 Mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Tanga mwaka wa kwanza.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Ramadhani Kingai amesema Mhanga alikamatwa kwa nguvu na kuingizwa ndani kisha kubakwa na vijana hao wakiwa wanne huku wakifungulia redio kwa sauti kubwa.

Kamanda Kingai amesema kuwa Mmoja ya Watuhumiwa aitwaye Bakari Hassani alikula njama na wenzake wengine walivyokaribia kwenye nyumba ambayo anaishi binti huyo walimkamata na hatimaye kumuingiza kwenye nyumba waliyomfanyia ubakaji huku wakiwa wamefungulia redio kwa sauti kubwa ili kelele za binti kuomba msaada zisisikike.


"Watuhumiwa hao walivyomaliza kitendo hicho walipomaliza walikimbia" amesema Kamanda Kingai

Kamanda Kinghai amewataja Watuhumiwa waliofanya ubakaji huo katika eneo la Mrusi kata ya Heruchuni Wilayani Kasulu kuwa ni Julius Yolemino(24), Hemed miosho (24) na Bakari Hassani(21) na Mtuhumiwa wa nne ambaye anafahamika kwa sura na aliyebakwa, bado anatafutwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages