Breaking

Sunday 3 July 2022

WATU SITA WA FAMILIA MOJA WAUAWA KIGOMA




Watu sita wa familia moja wameuawa kwa kukatwa sehemu mbalimbali za miili yao kwa kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Kiganza wilayani Kigoma mkoani Kigoma.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Menrad Sindano amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Julai 3, 2022.

Sindano amesema katika mauaji hayo watoto wawili wamejeruhiwa, mmoja mwenye miezi mitatu na mwingine mwenye umri wa miaka minne, ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali kuweza kuwabaini watu waliofanya mauaji hayo na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa watakaobainika kuhusika na tukio hilo.

“Kulingana na aina ya mauaji haya tunaona kabisa si mtu mmoja aliyeweza kufanya tukio hilo hivyo inawezekana ni mtu zaidi ya mmoja kwani wote walikuwa katika vyumba vyao vitatu na miili imekutwa humo katika vyumba hivyo walipokuwa wamelala watu hao,”amesema kaimu Kamanda Sindano.


Source: Mwananchi 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages