Breaking

Tuesday 16 August 2022

DC MKUDE AKABIDHI VIFAA KWA KIKUNDI CHA WANAWAKE WAGONGA KOKOTO KISHAPU



Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe Joseph Modest Mkude amekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi laki 6 kwa kikundi cha kina mama cha "Kazi iendelee" kinachojihusisha na shughuli ya kugonga kokoto kilichopo katika kata ya mwadui Luhumbo Halmasauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

DC Mkude amekabidhi vifaa hivyo jana jumatatu August 15, 2022 alipokuwa katika Ziara yake ya kikazi katika kata hiyo ambapo aliambatana na Afisa maendeleo wa wilaya ya Kishapu.

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo aliwaelekeza wanakikundi kutunza vifaa hivyo ili viwasaidie katika kurahisisha kazi ya upigaji wa kokoto ili viwaletee manufaa zaidi na hatimaye kununua vifaa vya kisasa zaidi.

“wanawake wanaweza kufanya kazi ya aina yoyote ili mradi tu wakiwekewa mazingira Mazuri kama vile mlivyonitaka mimi niwatafutie vifaa hivi ni vifaa vya kuanzia lakini serikali yenu ipo tutajitahidi kuwaletea vifaa vya kisasa zaidi katika utendaji wenu kazi ambapo nyie mnajishugulisha na uchimbaji madini ujenzi (MAWE) kwa kuyafanya yawe kokoto Mkurugenzi yupo kupitia idara ya Maendeleo ya jamii Tunaomba Vikundi hivi aendelee kuvisajili na kuvitafutia mikopo” amesema Dc Mkude

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mwadui Luhumbo Mhe Francis Manyanda Amemshukuru sana na kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kishapu kwa Moyo wa Upendo alio uonyesha kwa wanakikundi wa kikundi cha Kazi iendelee kilichpo ndani ya kata yake

“Tunakushukuru sana Mkuu wa Wilaya kwa kutoa msaada wa Nyundo hizi kwa kina Mama hawa kwani itawarahisishia katika utendaji kazi wao, mwanzo walikuwa wakihangaika na kuokoteleza ma vyuma ambayo muda mwingine yamekuwa yakiwaumiza mikono kwa Nyundo hizi zitawasaidia kuleta maendeleo ya Wilaya na ya kwao na familia zao" amesema Diwani Manyanda

Aidha amemuomba Mkuu wa Wilaya kufanya jitihada za kuwatafutia soko la uhakika la kokoto wanawake hao ili waweze kunufaika kiuchumi.

Akitoa pongezi na Shukran, Katibu wa kikundi cha Kazi indelee Sophia selemani amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutumiza ahadi yake ya kutoa vifaa hivyo ambavyo vitawasaidi katika uchimbaji madini (MAWE)

“Kwenye chimbo letu tulikuwa na changamoto ya vifaa tuliomba kwa Mkuu wa wilaya msaada wa Nyundo ambazo zitatusaidia kurahisisha kazi zetu za kooto leo hii tunamshukuru sana Mkuu wetu wa Wilaya kwa kutuletea vifaa hivi ambavyo kwa kiasi kikubwa kitatusaidia wanaikundi kuzalisha kokoto kwa wingi"

Katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude aliwakumbusha wananchi swala la Sensa ambalo litaanyika siku ya Jumanne ya Tar 23 mwezi wa Nane 2022 kuwa tayari kuhesabiwa na kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa ili kurahisisha zoezi la Sensa ya watu na Makazi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages