Breaking

Wednesday 17 August 2022

TANESCO YAAHIRISHA ZOEZI LA KUZIMA MFUMO WA KUNUNUA LUKU



Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limetangaza kuahirisha zoezi la kutengeneza kinga kwenye kanzi data ya mfumo wa LUKU ambalo lingesababisha kutokupatikana kwa huduma za kununua umeme wa LUKU kwa siku nne kuanzia August 22 mpaka 25.

Taarifa ya TANESCO imesema "TANESCO inawataarifu Wateja wake kuhusu kuahirishwa kwa zoezi la matengenezo kinga kwenye mfumo wa LUKU kama ilivyotangazwa mapema leo, tutawajulisha pale tutakapokuwa tayari kuendelea na zoezi hilo, Shirika linaomba radhi kwa usumbufu uliotokea"


TAARIFA YA AWALI

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages