Breaking

Monday 15 August 2022

WAFANYABIASHARA WAITWA KUSHIRIKI MAONYESHO YA AFRIKA MASHARIKI MWANZAWafanya biashara wameombwa kujitokeza katika maonesho ya biashara ya afrika mashariki ambayo hufanyika Mkoani Mwanza yanayotarajia kuanza August 26, hadi Septemba 4 katika viwanja vya michezo Nyamagana.

Hayo yamesemwabna Mwenyekiti wa TCCIA Gabriel Chacha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo hii ametoa wito kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo ya kujitangaza.

Chacha amesema kuwa miongoni mwa bidhaa zitakazo kuwepo katika maonesho hayo ni bidhaa za machine na Tekinolojia ,bidhaa za kilimo na mifugo, na ameongeza kuwa miongoni mwa Nchi ambazo zitahudhuria ni Kenya,Uganda na Rwanda.

Na kauli mbiu ya mwaka huu ni lugha ya kiswahili nguzo ya kukuza na kuendeleza biashara ,viwanda na kilimo Afrika.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages