Breaking

Friday 9 September 2022

MWANAFUNZI WA CHUO AUAWA KWA KISU DODOMA, WIVU WA MAPENZI WATAJWA



Winfrida Michael (24) mwanafunzi wa Chuo cha St John amefariki baada ya kuchomwa kisu na mpenzi wake Julias Gervas (26) ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho sababu ikitajwa kuwa wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa baada ya Julius kufanya mauaji hayo alijaribu kujiua kwa kujikata tumbo na sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Dodoma.

Ofisa muuguzi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Ester Ngoloki amesema Septemba 7, 2022 walimpokea Julias akiwa na jeraha la kuchomwa na kitu chenye ncha kali tumboni.

Amesema walimpokea Winfrida akiwa amefariki na mwili wake ukiwa na majeraha ya kitu chenye ncha kali.

“Majeruhi yupo hospitali akiendelea kupatiwa matibabu na anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji na mwili wa Winjfrida umechukuliwa na ndugu kwa ajili ya taratibu za familia,” amesema.

Source: Mwananchi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages