Breaking

Tuesday 6 September 2022

MAFUTA YASHUKA BEI, TAZAMA BEI KATIKA MIKOA YOTE HAPA



Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za ukomo wa mafuta kwa Septemba zitakazoanza kutumika kesho Jumatano.

Hii ni habari njema kwa watumiaji wa vyombo vya moto baada ya miezi kadhaa bei kupanda.

Kabla ya tangazo hili, bei ya petroli ni 3,410 huku dizeli ikiuzwa shilingi 3,322 kwa lita.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Septemba 5, 2022 na Mkurungenzi Mkuu wa Ewura, Modestus Lumato, kuanzia kesho Jumatano Septemba 7 petroli itauzwa kwa Sh 2, 969, dizeli Sh3, 125 na mafuta ya taa yatauzwa Sh 3,335 bei hizi ni kwa mkoa wa Dar es Salaam baada ya ruzuku ya Serikali.

Kushuka kwa bei za bidhaa hizo kunatokana na kupungua kwa bei za mafuta katika soko la dunia.
















Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages