Breaking

Tuesday 20 September 2022

UTEKELEZAJI MIRADI YA KUPENDESHA MIJI (TACTIC) KUANZA NA MIJI 12



OR -TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amesema hatua za awali za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina zimekamilika katika miji 12 kati ya 45 ya awali itakayonufaika na miradi ya kuboresha miundombinu katika Miji, Manispaa na Majiji

Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo Septemba 20, 2022 Bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa majibu ya maswali ya waheshimiwa wabunge kuhusu hatua za utekelezaji wa Miradi ya Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness (TACTIC).

“Usanifu katika miji 12 tayari umekamilika, kazi ya kutangaza tenda kwa ajili ya kupata wakandarasi itafanyika muda wowote ili kazi zianze Mwezi Machi b2023” amesema bBashungwa

Bashungwa amesema utekelezaji wa miradi hii ya TACTIC umegawanyika katika Makundi matatu, ambapo kundi la kwanza ni Miji ya Arusha CC, Mwanza CC, Dodoma CC, llemela MC, Kigoma MC, Mbeya CC, Geita TC, Morogoro CC, Songea MC, Sumbawanga MC, Tabora MC na Kahama MC.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan alielekeza kuwa baada ya Serikali kusaini Mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia mradi utaratibiwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI mwezi Juni 2022, alielekeza utekelezaji wa Miradi huo kuanza mara moja.

Aidha, Bashungwa amesema utekelezaji wa miradi hiyo katika kundi la kwanza utaenda sambamba na kundi la pili litakalohusisha miji 15 ambayo ni Mtwara Mikindani MC, Tanga CC, Babati TC, Bariadi TC, Bukoba MC, Iringa MC, Kibaha TC, Korogwe TC, Lindi MC, Moshi MC, Mpanda MC, Musoma MC, Njombe TC, Singida MC na Shinyanga MC

Vile vile, amesema utekelezaji wa miradi ya TACTIC kundi la tatu utafanyika katika mwaka wa fedha wa 2022/ 2023 katika miji ya Bunda TC, Handeni TC, Ifakara TC, Kasulu TC, Kondoa TC, Mafinga TC, Makambako TC, Masasi TC, Mbinga TC, Mbulu DC, Nanyamba TC, Newala TC, Nzega TC, Tarime TC, Tunduma TC, Vwawa TC, Bagamovo DC, Chato DC.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages