Breaking

Friday 30 September 2022

BRELA YAKITA KAMBI MAONESHO YA MADINI GEITA



Na Samir Salum, Lango la Habari
 

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA imewaasa wananchi wa Mkoa wa Geita na Mikoa ya jirani kutembea kwenye banda lake lililopo kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Bombambili, mjini Geita.

Mkuu wa kitengo cha uhusiano wa BRELA Bi.Roida Andusamile amesema kuwa uwepo wa BRELA katika maonesho hayo ni fursa kwa wafanyabiashara kujitokeza ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo Kurasimisha biashara zao, kupata leseni za Biashara na viwanda na kuhuisha majina ya biashara.


Bi. Andusamile amesema tangu kuanza kwa maonesho hayo September 27, 2022 wafanyabiashara wengi wametatuliwa changamoto zao huku wadau wengi wakifanikiwa kupata vyeti vya Usajili ambavyo vinatolewa papo Kwa papo.

“tumegundua wengi wanapata changamoto katika kuingia kwenye mtandao hivyo kupitia banda hili tunawasaidia na kutatua changamoto zao.” Amesema



Zaidi ametaka wadau kujitokeza Kwa wingi kwani Walala umejipanga kutoa huduma Kwa  haraka na ufanisi zaidi huku akisisitiza kuwa BRELA imeweka mazingira rafiki Kwa wadau wote kupata huduma

Bi Andusamile ametumia  fursa hiyo kuwataka wadau kufika katika Banda la BRELA ili kupata elimu stahiki kuhusu urasimishaji wa Biashara na kuacha kuwatumia watu wa kati ambao huchelewesha maombi yao ya usajili.

Maonesho ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye Viwanja vya Bombambili Mjini Geita yameanza September 27, 2022 na yanatarajia kufika kilele Oktoba 08, 2022.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages