Breaking

Sunday 16 October 2022

WANANCHI KAKONKO WATAKIWA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA AFYA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kuhakikisha wanatunza miundombinu ya afya inayojengwa na serikali ili idumu kwa muda mrefu.


Rais Samia ameyasema hayo leo Oktoba 16, 2022 alipokuwa akizimdua Hospitali ya Wilaya ya Kakonko, Halmashauri ya Wilaya ya Kankoko,mkoani Kigoma iliyojengwa kwa gharama ya Sh.bilioni 2.9.


"Wito wangu kwenu ni kutunza mali yenu, hii si mali ya Serikali, jitahidini kutunza hospitali yenu iwahudumie leo, kesho na kesho kutwa," amesisitiza Rais Samia.


Amesema serikali itaendelea kununua vifaa tiba vya vipimo vyote vinavyohitajika kw binadamu pale anapotakiwa kuhudumiwa.


Amesema kuwa vifaa tiba vimenunuliwa lakini bado vingine havipo, hivyo serikali itahakikisha inaleta vifaa kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages