Breaking

Friday 14 October 2022

MZEE ADAIWA KUMBAKA MWANAFUNZI KWA ELFU KUMI



Mzee Aboubakar Said (64), mkazi wa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza baada ya kumrubuni kwa kumpa shilingi elfu 10.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Jackson Mwakagonda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mtuhumiwa huyo alifanya kitendo hicho cha ukatili Oktoba 10, 2022 majira ya saa 8:00 mchana

Kaimu Kamanda Mwakagonda, amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikamatwa na uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria huku akiwataka wazazi na walezi kuimariha ulinzi kwa watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili.

Source: EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages