Breaking

Friday 14 October 2022

AMUUNGUZA KWA MAJI YA MOTO USONI MKE MWENZA



Siku ya Jumatano, Oktoba 12, mwanamke alikamatwa kwa kumshambulia na kumchoma mke mwenza usoni na maji moto wakati wa mazishi katika kijiji cha Dede, Awendo, Kaunti ya Migori.

Mwanamke huyo alichukua fursa hiyo kutenda unyama huo, baada ya mwathiriwa kuhudhuria mazishi hayo. 

"Hakuwa anaonekana akona shida yoyote, kwa hivyo tulifikira kuwa yuko sawa na uwepo wa mke mwenza, hatukujua anaweza kufanya kitendo kama hicho," Veronica

Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Awendo Mathias Pombo alisema mshukiwa aliolewa kama mke wa pili baada ya mke wa kwanza kuondoka baada ya tofauti za kifamilia.

"Tukio hili lilitendeka wakati wa matanga ya jirani. Mshukiwa yuko kizuizini na atapelekwa mahakani Alhamisi," Pombo alisema

Iinadaiwa kuwa mwathiriwa aliachana na mume wake miaka saba iliyopita, na kurejea siku hiyo kuifariji familia iliyofiwa ndipo akakutana na kisirani hicho.

Polisi wanasema inaonekana mwanamke huyo alikerwa na jinsi mke mwenza alivyotangamana na mumewe ndipo akaamua kumuadhibu.

"Ninafikiri mshukiwa hakupenda jinsi mke mwenza alivyotangamana na mumewe ndipo akaamua kumshambulia," Pombo aliongeza kusema.

Mwathiriwa alijeruhiwa usoni kwa kuchomeka vibaya, na kukimbizwa katika Hospitali ya Misheni ya Ranen ambako anaendelea kutibiwa.

Mshukiwa naye anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Awendo, huku uchunguzi ukiendelea ili afikishwe mahakamani.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages