Breaking

Tuesday 25 October 2022

POLISI AVAMIA SHULE AMCHOMA KISU MHASIBU AKIDAI KURUDISHIWA ADA



Afisa wa polisi wa Kitui nchini Kenya ametiwa mbaroni baada ya kuvamia shule ya upili ya wasichana huko Mwingi na kumdunga kisu mhasibu.

Karao huyo, Haji Boru, anasemekana kufika kwa hasira katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Mwingi, akitaka kurejeshewa karo ya ziada zinazolipwa kupitia Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge.

Katika ripoti ya Citizen TV, mhasibu aliyeathiriwa ilieleza kuwa pesa hazingeweza kurejeshwa lakini zingeweza kuhamishwa kwa karo ya chuo kikuu cha mwanawe, lakini afisa aliyeshtakiwa hakutaka kusikia hilo.

Mara moja alichomoa kisu na kumdunga mhasibu huyo aliyetambulika kwa jina la Alex Mwanzia.

OCPD wa Mwingi ya Kati Peter Mutuma alithibitisha kisa hicho akisema mshukiwa alikuwa amewekwa korokoroni na sasa anasubiri kufikishwa mahakamani.

Mhasibu huyo kwa sasa amelazwa hospitalini kupokea matibabu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages