Breaking

Wednesday 26 October 2022

WAZIRI BASHUNGWA ALIPONGEZA JESHI KWA ZOEZI LA DRAGON FLY



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa amepongeza mafanikio Zoezi la Kamandi ya Jeshi la Anga lijulikanalo kama ‘Dragonfly’ linalofanyika eneo la Mitwero mkoani Lindi.

Ameyasema hayo wakati alipotembelea kujionea Zoezi hilo la siku kumi kwa kuhusisha zana za Kamandi ya Jeshi la Anga zikiwemo ndegevita, ndege za usafirishaji, helikopta, mizinga ya kudungulia ndege, makombora pamoja na RADAR.


Akihutubia umati wa watu waliofika kushuhudia zoezi hilo, Waziri Bashungwa amepongeza jitihada zilizofanyika kuandaa za kuandaa zoezi hilo, ambalo linahusisha Idara za huduma, wataalamu wa zana za ulinzi wa anga kwa maana ya mizinga ya kudungulia ndege, makombora, radar na ndegevita.

Aidha, Waziri Bashungwa ameongeza kwa kusema kuwa wote ni mashuhuda, kwa jinsi ambavyo wameona zana mbalimbali zinavyoweza kuunganisha mapigo, kuelekea kwenye shabaha (target).

“Hiki ni kielelezo cha mafunzo bora, sambamba na mpango mzuri wa utunzaji wa zana, naamini mafanikio ya zoezi hili hayakuwa rahisi, kwani lilihitaji moyo wa kujituma na weledi wa hali ya juu” amesema Bashungwa



Kuhusu kufanya mazoezi ya pamoja, Waziri Bashungwa anaamini kuwa katika mipango yao iko dhana ya kufanya mazoezi ya pamoja yatakayohusisha Kamandi zote (Joint Exercises).

“Mazoezi ya kuhusisha Kamandi zote, ni utaratibu ambao unatoa picha nzuri ya kuona utayari wa majeshi yetu kwa ujumla, Ni fursa ya kujipima utayari wetu ni wa kiwango gani, na wapi tufanye marekebisho ili kijiimarisha zaidi kwa ajili ya kukabiliana na adui na kumshinda”


Waziri Bashungwa amepongeza kwa uchaguzi wa eneo wa eneo la kufanyia zoezi hili, maana anaamini mazoezi kama haya yatawazoesha marubani wetu kuruka maeneo tofauti tofauti, ili kuweza kujua kwa kina jiografia ya nchi yetu, jambo ambalo litawafanya kuwa tayari wakati wote.

Vile vile, amesema anaamini kuwa jukumu la kuhakikisha zana na vifaa vyetu vinkuwa tayari muda wote ni endelevu. Kwa maana hiyo, na amewaasa wanakamandi wote waliopewa dhamana ya kutunza zana hizi, kuhakikisha zinatunzawa na kufanyiwa matengenezo yanayohitajika kwa wakati.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages