Breaking

Thursday 20 October 2022

MAMBO SITA YA KUPATA MAFANIKIO YA MICHEZO KWA WANAWAKE HAYA HAPA



Na John Mapepele

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amevitaka Vyama na Mashirikisho ya Michezo kuwa na dhana ya kujitangaza huku akilielekeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kushirikiana na vyama kuratibu mafunzo maalum kwa maafisa Habari ili waweze kujitangaza na kupata mafanikio.

Dkt. Abbasi ameyasema haya kwenye Kongamano la Kimataifa la Michezo kwa Wanawake wakati akitoa mada ya jinsi ya kuvitumia vyombo vya Habari kimkakati kutangaza vyama na Mashirikisho ili kupata wadhamini.

Ameyataja mambo ya kusukuma michezo kisayansi kuwa ni pamoja kutumia mitandao ya kijamii ya kidigitali kwa kuwa dunia ipo kiganjani.

Akinukuu baadhi ya watu maarufu duniani kama Bill Gate amesema wamekuwa wakisisitiza uwekezaji wa kujitangaza ili kupata mafanikio.

Dkt. Abbas Ametaja mambo mengine kuwa ni utawala bora na uwazi na amesema Wizara tayari imefungua madarasa kwenye Chuo cha michezo cha Mallya mwanza na tawi la Dar es Salaam ambapo ametoa wito kwa Mashirikisho kwenda kujifunza.

Aidha, amevitaka Vyama na Mashirikisho hayo kuwa na mikakati ya mawasiliano itakayosaidia kutoa dira na kufanya tathmini ya jinsi vinavyojitangaza.

Pia kutumia Vyombo vya Habari vya kijamii kama redio na televisheni kwa kuwa vina vipindi vya bure ambavyo vitasaidia kutangaza Mashirikisho hayo.

Aidha, amesema Tamasha hili maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo alielekeza kuwaendelea kufanyika kila mwaka ili kuinua vipaji vya Wanawake hapa nchini.

Amefafanua kuwa dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuendelea kutumia michezo kuitangaza Tanzania duniani.

Katika hatua nyingine amezipongeza timu za taifa za soka za Wanawake (Serengeti girls) na Watu wenye Ulemavu ( Tembo Warriors) kwa kushiriki kwenye mashindano ya Kombe la Dunia na kufika hatua ya robo fainali na kuyataka Mashirikisho kuiga mifano hiyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages